KISWAHILI

UUMALI ni nini?
UUMALI ni Umoja wa Utunzaji wa Msitu Lijala.

Kwa nini UUMALI ilianzishwa?
Kwa sababu ya uhifadhi wa msitu asili lijala na ufugaji nyuki ,kuhamasisha jamii katika ufugaji wa nyuki naa uhifadhi msitu wa asili na ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Shughuli za UUMALI ni zipi?
Uhifadhi wa msitu wa asili na ufugaji nyuki.

Ninawezaje kushiriki?
Kuomba maombi ya kujiunga na kikundi kwa uongozi wa kikundi.

UUMALI iko wapi?
Mkoa wa Lindi,wilaya ya Lindi Mtaa wa (LIJALA -RUAHA na Kijiji cha Mandawa-Kiwalala.

ENGLISH

What is UUMALI?
UUMALI is the Community Forest Conservation Association of Lijala.

Why was UUMALI established?
Due to the conservation of the Lijala natural forest and beekeeping, to raise community awareness on beekeeping and natural forest conservation as a way to address climate change.

What does UUMALI do?
Conservation of natural forests and beekeeping.

How can I participate?
Applying to join the group through the group leadership.

Where is UUMALI located?
Lindi Region, Lindi District, Lijala-Ruaha Street and Mandawa-Kiwalala Village.

Dira , Dhima na Malengo


🌳Dira

Kuwa mlinzi wa misitu asili na mazingira safi, salama na yanayovutia jamii kuishi kwa utulivu, huku tukipunguza majanga yatokanayo na uharibifu wa mazingira.

🐝Dhima

Kushirikiana na serikali, mashirika na jamii katika kuhamasisha, kuelimisha na kutetea uhifadhi wa misitu kwa njia za mila na desturi zenye mwelekeo endelevu wa mazingira.

📚Malengo

  • Kuhifadhi msitu wa asili wa Lijala.
  • Kutumia rasilimali kwa kuzingatia kanuni za uhifadhi.
  • Kuendeleza upandaji miti rafiki kwa mazingira.
  • Kutoa elimu ya utunzaji wa misitu.
  • Kuhamasisha ufugaji bora wa nyuki.

Vision , Mission and Objectives


🌳Vision

To be a guardian of natural forests and a clean, safe, and attractive environment that promotes peaceful community living, while reducing disasters caused by environmental destruction.

🐝Mission

To collaborate with the government, organizations, and communities in promoting, educating, and advocating for forest conservation through traditional and cultural practices that support sustainable environmental management.

📚Objectives

  • To conserve the Lijala natural forest..
  • To utilize natural resources in accordance with conservation principles.
  • To promote the planting of environmentally friendly trees.
  • To provide education on forest conservation.
  • To promote sustainable beekeeping practices.

KAULI MBIU

" Kuhifadhi Mazingira ya kitamaduni kwa kizazi endelevu"